Leo tarehe, 27 /02 /2015 Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) ikishirikiana na Friends of Fatema pamoja na Mtanzania Jitambue (MJ). Tumetoa Msaada wa kufanya FUMIGATION kwenye mabweni manne katika WATOTO wenye ULEMAVU wa Ngozi Kambi ya BUHANGIJA SHINYANGA mjini. Hivyo basi kutokana na mchango nilioomba kuchangisha kwa radhaa za maadimin ili kuwasaidia watoto hao wenye mazingira magumu, jumla ya pesa taslimu Tsh.305,000/= zilipatikana na kiasi cha Tsh.190,000/= ndio kilichotumika kwa FUMIGATION hiyo. Aidha kiasi cha Tshs.110,000/= kilichobaki kimetumika kufanya maintanance ya miundo mbinu ya maji kambini hapo ambapo walikua wanakosa maji safi na salama ya bomba kwa ubovu wa koki 4 za maji pia Mabweni 2 yalikua hayana umeme na fundi amaendelea na kutengeneza. sambamba na hilo pesa kidogo iliyo baki imetumika kununua catton ya sabuni za kufulia na sukari kilo 5.
Sambamba na hayo pia nimekabidhi nguo za watoto wa kike pieces 86 na nguo za kiume pieces 18 ambazo zilitumwa na Dk.Shaban(Aluta) kwa niaba ya Friends of Fatema.
Haya yote yamekwenda sambamba na kufanya usafi katika Kambi hiyo kama agizo la Rais linavyoelekeza kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Kwa niaba ya WATOTO napenda kutoashukrani za dhati kabisa kwa wakioguswa na ombi langu kwani chamgamoto ya kunguni kwao limetatuliwa kutokana na mchango wetu wa hiari.
Mpatapo nafasi mfike kambini mjionee.
ASANTENI SANA
Ndg.Andrew Malulu
Kwa niaba ya Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania, Friends of Fatema na Mtanzania Jitambue